Home NECTA DOCS Uchambuzi wa Majibu ya Watahiniwa katika Mtihani wa Kiswahili wa Kidato cha...

Uchambuzi wa Majibu ya Watahiniwa katika Mtihani wa Kiswahili wa Kidato cha Nne mwaka 2022

201
0
SHARE
Items Response Analysis (CIRA) report for the Certificate of (CSEE), in the Geography subject 2022.
Uchambuzi wa Majibu ya Watahiniwa katika Mtihani wa Kiswahili wa Kidato cha Nne mwaka 2022

Uchambuzi wa Majibu ya Watahiniwa katika Mtihani wa Kiswahili wa Kidato cha Nne mwaka 2022

Kiswahili CIRA  for 2022, Vitabu vya uchambuzi majibu ya wanafunzi CIRA 2022, CIRA for Kiswahili 2022,  Students Item Response Analysis Report, CIRA CSEE, CIRA CSEE 2022, NECTA CIRA FOR CSEE, CSEE CIRA 2022, CIRA CIVICS 2022, Candidates Item Response Analysis Report CSEE 2022

Taarifa ya Uchambuzi wa Majibu ya Watahiniwa katika Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne mwaka 2022 imeandaliwa ili kutoa mrejesho kwa wanafunzi, walimu, watunga sera, wakuza mitaala na wadau mbalimbali wa elimu kuhusu matokeo ya watahiniwa katika somo la Kiswahili kwa ujumla.

Taarifa hii ni tathmini ya mwisho inayolenga kuonesha mafanikio ya mfumo wa elimu katika mchakato mzima wa ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Kiswahili kwa watahiniwa wa Kidato cha Nne. Kimsingi uchambuzi wa majibu ya watahiniwa katika mtihani huu unalenga kuonesha dhahiri maarifa ambayo mfumo wa elimu uliweza au haukuweza kuwapa watahiniwa katika somo la Kiswahili kwa kiwango cha Sekondari, Kidato cha Kwanza hadi cha Nne.

Uchambuzi uliowasilishwa katika taarifa hii una lengo la kuonesha sababu za watahiniwa kufanya vizuri, vibaya au kwa kiwango cha wastani katika maswali/mada mbalimbali zilizopimwa.

Ripoti hii inaonesha baadhi ya sababu zilizofanya watahiniwa kufanya vizuri kama vile kuwa na uelewa mzuri wa mada na uzingatiaji mkubwa wa matakwa ya swali.

Pia sababu za watahiniwa kuwa na kiwango cha wastani cha ufaulu zimeelezwa kuwa ni pamoja na kutoa majibu yasiyojitosheza.

Aidha, sababu zilizofanya watahiniwa wachache kupata alama hafifu katika majibu yao zimefafanuliwa kama vile kutoelewa matakwa ya swali, uwezo mdogo wa kuelezea dhana mbalimbali kwa ufasaha, na udhaifu katika kuelewa dhana zinazohusiana na somo la Kiswahili kwa ujumla.

Uchambuzi wa Majibu ya Watahiniwa katika Mtihani wa Kiswahili wa Kidato cha Nne mwaka 2022

Baraza la Mitihani lina imani kuwa, mrejesho uliotolewa utawawezesha wadau wote wa elimu kuchukua hatua madhubuti za kuboresha mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji, hatimaye kuondoa changamoto zilizobainishwa katika taarifa hii.

Pia Baraza linaamini kuwa, mapendekezo yaliyotolewa mwishoni mwa taarifa hii yakizingatiwa ipasavyo, kiwango cha ufaulu katika somo hili kitakuwa bora zaidi katika mitihani ijayo inayotolewa na Baraza la Mitihani.

Taarifa hii inachambua viwango vya ufaulu wa watahiniwa katika mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2022 kwa somo la Kiswahili.

Mtihani huo ulikuwa na jumla ya maswali 12 yaliyogawanywa katika sehemu A, B na C kutoka katika mada za Ufahamu, Matumizi ya Sarufi, Utumizi wa Lugha, Uandishi, Maendeleo ya Kiswahili, pamoja na Fasihi.

Watahiniwa walitakiwa kujibu maswali yote katika sehemu A na B, na maswali matatu (3) kutoka sehemu C.

Viwango vya ufaulu wa watahiniwa vilipangwa katika madaraja mbalimbali ya ufaulu ambapo daraja A hadi D yalitumika kuwakilisha asilimia ya ufaulu wa watahiniwa waliopata alama 30 na zaidi.

Aidha, daraja F lilitumika kuwakilisha asilimia ya ufaulu wa watahiniwa waliofeli yaani waliopata alama chini ya 30.

Jedwali Na. 1 linaonesha ulinganifu wa ufaulu wa watahiniwa kwa kila daraja kwa mwaka 2021 na 2022.

 

DOWNLOAD/PAKUA PDF FILE

Uchambuzi wa Majibu ya Watahiniwa katika Mtihani wa Kiswahili wa Kidato cha Nne mwaka 2022

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here